School Rules

KANUNI NA TARATIBU ZA SHULE

  • Mwanafunzi anatakiwa asome na afaulu apate wastani zaidi ya 51
  • Mwanafunzi anapaswa kuongea kiingereza muda wote awapo shuleni.
  • Mwanafunzi anapaswa kuhudhuria vipindi vyote na kufanya kazi zote, nadharia na vitendo kama atakavyoelekezwa na mwalimu/msimamizi wake.
  • Mwanafunzi anapaswa kusimama na kusalimia watu wote wanaomzidi umri.
  • Mwanafunzi anapaswa kujifunza kuimba kwa usahihi na ukakamavu nyimbo zote rasmi za Taifa na shule
  • Mwanafunzi anapaswa kutii kwa hiari alama rasmi za Taifa na shule kama vile Bendera.
  • Mwanafunzi anapaswa kutumia lugha rasmi, isiyo na matusi wala kashfa kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo.
  • Mwanafuzi anapaswa kutoa taarifa za uharibifu wa mali yake binafsi, wenzake au shule kwa viongozi wake na waalimu.
  • Mwanafunzi haruhusiwi kuwasiliana na mtu yeyote ikiwa ni pamoja na wazazi kwa namna yoyote bila kibali  kutoka kwa mwalimu husika.
  • Mwanafunzi haruhusiwi kuuza kitu chochote au kufanya biashara yeyote awapo shuleni.
  • Mwanafunzi haruhusiwi kutoka nje ya eneo la shule bila ruhusa kutoka kwa mwalimu anayehusika, akionekana atachukuliwa hatua za kinidhamu.
  • Mwanafunzi haruhusiwi kutumia kilevi cha aina yeyote kama vile pombe, madawa ya kulevya n.k.
  • Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa nguo, viatu au urembo usioruhusiwa shuleni.
  • Ni marufuku mwanafunzi kuwa na simu ya mkononi, vipodozi na silaha ya aina yeyote.
  • Mwanafunzi haruhusiwi kujihusisha na vitendo viovu vifuatavyo:- Ngono. Mgomo wa adhabu au vinginevyo. Kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
  • Mwanafunzi hapaswi kujihusisha na vitendo vyovyote vya uchochezi.
  • Mwanafunzi hapaswi kubagua wenzake kwa vigezo vya dini, kabila, rangi na utaifa n.k.
  • Mwanafunzi haruhusiwi Kufanya udanganyifu wa aina yoyote katika mitihani kama kuibia kwa mwanafunzi mwenzake; kuingia chumba cha mtihani na karatasi, nguo au vitambaa vilivyo na maandishi; kuwasiliana na mwanafunzi mwenzake kwenye chumba cha mitihani wakati mtihani ukiendelea; n.k.
  • Mwanafunzi haruhusiwi Kupigana na wanafunzi, wafanyakazi au watu wengine
  • Mwanafunzi haruhusiwi kuingia shuleni na chakula chochote labda kwa idhini ya uongozi wa shule.

Mwanafunzi akivunja kanuni na taratibu za shule atachukuliwa hatua za kinidhamu